
Wakulima wameyasema hayo kwenye kongamano la miaka 61 ya uhuru mkoani Geita na kuiomba serikali iweze kuleta miradi ya umwagiliaji Maji ili waweze kufanya kilimo chenye kuleta maendeleo kwa jamii
"Kwa upande wa kilimo tunashukuru kinaendelea lakini sasa upande wa hali ya hewa, tabia ya nchi inachanganya na bei zinachanganya yani sisi wakulima wakati mwingine tunapata kikwazo kidogo kwa sababu ya utaratibu bei hazijawa Sawa sawa, hapo serikali ijitathimini vizuri kusudi wakulima tupate nafasi nzuri ya kupata mapato mazuri, kutuongezea Mbolea na kutuwaishia Mbolea kabla hatujaanza kilimo", alisema Nkingwa.
"Miaka 61 imepiga hatua kubwa sana kuna maendeleo mazuri na tunaomba viongozi wetu waweze kujikita kwenye maendeleo ili watanzania waweze kunufaika", alisema Thomas
Afisa mipango halmashauri ya mji Geita Ndalo Samson anasema kutokana na mabadiliko ya tabia ya nchi zao kuu la biashara (Pamba), limeendelea kushuka huku akitoa ushauri wa mazao mbadala yatakayoendana na mabadiliko ya tabia ya nchi.
"Hali ya uzalishaji wa zao hili umekuwa ukishuka mwaka hadi mwaka kutokana na mabadiliko ya tabia ya nchi na bei ya soko la dunia hata hivyo wananchi wanahanasishwa kulima mazao mengine mbadala ya biashara hasa zao la Alizeti", alisema Samson.
Mkuu wa wilaya ya Geita Wilson Shimo amewataka wananchi kuwa wamoja ili serikali inapoleta miradi ya maendeleo iweze kufanikiwa kwa urahisi.
"Tukibaguana tukatengana tukasema huyu ni mtaalam, tukasema huyu ni mwanasiasa tukasema huyu ni wakike huyu wakiume, tukasema huyu ni mkristo huyu kuislam, huyu ni wa bara huyu ni wa visiwani na huyu wa CCM huyu wa Chadema tunakwenda kubaguana kusiko na sababu kwahiyo tusitengwe na vitu hivi ambavyo nimevitaja", alisema Shimo