Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Wakala wa Meli Tanzania waunga mkono DP World

Jumatano , 28th Jun , 2023

Chama cha Wakala wa Meli Tanzania (TASAA) kimeunga mkono mpango wa Serikali wa kuleta uwekezaji wa kampuni ya DP World kwenye bandari ya Dar es Salaam, kikisema kuwa uwekezaji huo utasaidia kuongeza ufanisi wa bandari na kukuza uchumi wa Tanzania.

TASAA imesisitiza kuwa DP World ni moja ya kampuni kubwa duniani za uendeshaji wa bandari ambazo zinaweza kuleta meli nyingi kuja Dar es Salaam, kuongeza idadi ya shehena inayohudumiwa na bandari na kuimarisha ufanisi wa bandari kwenye kuhudumia shehena.

Mwenyekiti wa TASAA, Daniel Mallongo, amesema kuwa kuna changamoto kadhaa za ufanisi kwenye bandari ya Dar es Salaam zinazolikosesha taifa mapato, ambazo zinatarajiwa kupatiwa ufumbuzi na uwekezaji wa DP World.

Alizitaja changamoto hizo kuwa ni pamoja na upungufu wa magati ya kuhudumia mizigo na kukosekana kwa mfumo wa kisasa wa kuhudumia mizigo bandarini kwa kasi.

"Ukosefu wa magati ya kutosha bandarini (Dar es Salaam) unasababisha meli kukaa nje siku 4 mpaka 6. Hii ni gharama kubwa kwa wenye meli kubwa za mizigo kwa sababu gharama ya kukaa pale nje (outer anchorage) ni Dola za Marekani 25,000 (Shilingi milioni 60) hadi Dola 50,000 (Shilingi milioni 120) kwa siku," alisema Mallongo.

"Ukiangalia meli inakaa siku 6 nje kabla ya kuhudumiwa, hiyo ni gharama kubwa. Na hizo gharama mara nyingi zinahamishiwa kwenye mizigo na kila mwenye mzigo kwenye hiyo meli ni lazima achajiwe gharama za meli kukaa nje."

Alisema pia kukosekana kwa mifumo inayosomana kati ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) na Mamlaka ya Mapato ya Tanzania (TRA) na uhaba wa nafasi ya kuhifadhia mizigo kwenye eneo la bandari ya Dar es Salaam ni changamoto nyingine kubwa.

"Haya mambo yote DP World ndiyo champion (kinara) wake. Ukimleta matatizo haya utapata ufumbuzi. Kama ni meli itakuja siku moja itandoka na ukipunguza gharama hiyo hata gharama ya kuleta mizigo Tanzania itashuka," aliongeza katika mahojiano na kituo cha EFM Redio na TV leo jijini Dar es Salaam.

"DP World ni kati ya kampuni kubwa tatu duniani ambazo zinaendesha bandari mbalimbali. DP World inaendesha takribani bandari 64 duniani, unaongelea Afrika, Asia, Ulaya na hata bara la Amerika. Kwa muktadha huo, DP World ina uwezo mkubwa."

Mwenyekiti huyo wa TASAA alizitaja Antwerp, London Gateway na New Jersey, kuwa miongoni mwa bandari zinazoendeshwa kwa ufanisi na DP World.

"Kwangu mimi niseme kwa uwazi kuwa DP World wana uwezo na wanastahili kuendesha bandari (ya Dar es Salaam)," alisisitiza.

Mallongo alisema faida ya uwekezaji wa DP World kwenye bandari ya Dar es Salaam ni kuwa utapunguza gharama za kupitisha mizigo na kuimarisha huduma na kufanya idadi ya shehena kuongezeka na hiyo itaongeza mapato kwa Serikali.

"Ukitaka kuongeza mzigo Dar es Salaam, lazima wenye meli wawe tayari kuja Dar es Salaam. Kama wenye meli wakiona kuna gharama za ajabu ajabu Dar es Salaam, wataenda kwa washindani wetu kama bandari za Maputo, Mombasa na Durban," alisema.

Kuhusu upotoshaji kuwa bandari ya Dar es Salaam imeuzwa kwa DP World au kukodishwa kwao milele au kwa miaka 100, kiongozi huyo wa TASAA aliwataka Watanzania wapuuze uongo unaoenezwa na baadhi ya wanasiasa na wanaharakati dhidi ya uwekezaji huo.

"Mimi siyo mwanasheria lakini najua kusoma. Unapoambiwa IGA au Intergovernmental agreement (illiyopitishwa na Bunge) ni framework (makubaliano tu ya msingi), mikataba yenyewe bado haijasiniwa," alisema.

HABARI ZAIDI

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko

Serikali yaipongeza Red Cross

Waziri wa TAMISEMI Mohamed Mchengerwa

Aonya wanaochangia watumishi kutopanda madaraja

Edgar Lungu, Rais wa Zamani Nchini Zambia Akitembea Kuzunguka Mji Mkuu wa Lusaka

Rais wa zamani Zambia Bw. Lungu hatarini kukamatwa

Mkuu wa Ulinzi Ukraine (Picha ya Website)

Zelensky amfukuza kazi mkuu wake wa ulinzi

Baadhi ya Wananchi wa Chindi na Ntinga wakiwa katika Harakati za Kuvuka Mto

Walazimika kulipa hadi 8000 kuvuka mto kwa mtumbwi

Mohamedi Mchengerwa, Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).

Wanaozuia watumishi kupanda vyeo wakaliwa kooni

Bujukano Mahungu John, Mwenyekiti wa Umoja wa Waganga na Wakunga wa Tiba Asili Tanzania

Waganga wa jadi waungana kukemea ukatili, Geita

Mhe. Kassim Majaliwa, Waziri Mkuu wa Tanzania

Mvua zilizoambatana na upepo zimeua watu watano TZ

Muonekano wa Eneo la Somanga baada ya Mawasiliano kati ya Lindi na Dar es Salaam kurejeshwa.

Mawasiliano yarejeshwa barabara ya Dar - Lindi