Alhamisi , 22nd Sep , 2022

Kampuni ya simu za mkononi nchini ya Vodacom imesema imepoteza takribani zaidi ya shilingi bilioni 103.9 tangu tozo za miamala ya simu kwa Vodacom ilipoanza mwezi wa saba mwaka jana hadi kufikia mwezi wa tatu mwaka huu.

Kaimu Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Vodacom Tanzania.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumaliza mkutano mkuu wa mwaka wa kampuni hiyo Kaimu Mkurugenzi wa Vodacom Hilda Bujiku amesema tozo zimesababisha miamala ya simu kushuka  upande wa mtu mmoja kwenda kwa mwingine na vile vile upande wa kutoa pesa kwa wakala kwa zaidi ya asilimia 30.

Kuhusu taarifa ya hivi karibuni iliyotolewa na waziri wa fedha akiwa bungeni kwamba tozo za miamala ya fedha zitapunguzwa kwa asilimia 10 mpaka 50 amesema inatia moyo kwao kama wawekezaji kwenye sekta ya mawasiliano kwa sababu ni kitu wamekuwa wakikisubiri.