Ijumaa , 16th Feb , 2024

Mkuu wa Idara ya masuala ya Kiuchumi (Head of Governance and Economic Section) kutoka Umoja wa Ulaya (EU) Karina Dzialowska, amesema kuwa Umoja wa Ulaya  utaendelea kushirikiana na Tanzania katika masuala ya kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji.

Hayo ameyabainisha alipokutana na kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Dkt. Tausi Kida na kujadiliana kuhusu namna wanavyoweza kuendelea kushirikiana katika kuibua mikakati mbalimbali inayolenga kuongeza uwekezaji nchini.

Aidha Karina alibainisha uwepo wa fursa ya upatikanaji wa fedha kwa ajili ya uwekezaji katika miradi rafiki kwa mazingira (Green investment) ambayo itatokana na fedha zinazopatikana kupitia masoko ya mitaji kwa amana mahsusi kwa ajili ya miradi rafiki kwa mazingira (Green Bonds).

Vilevile, katika kikao hicho viongozi hao wamezungumzia  utekelezaji wa mpango wa maboresho ya mazingira ya Biashara na Uwekezaji (BLUE PRINT) unaofadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU) kupitia mradi wa Business Environment Growth Innovation (BEGIN)