Jumatatu , 27th Jun , 2022

Wafanyabiashara wa nafaka katika soko la Tandale Dar es Salaam wamesema hali ya bei za nafaka itazidi kupanda juu kutokana na ukame kwa baadhi ya mikoa inayolima mazao ya nafaka ikiwemo Michele, Maharage na mahindi.

Katika Kilo moja ya mchele kwa sasa inauzwa Hadi Shilingi 2300 Maharage yakiuzwa Hadi Shilingi 2200 ambapo wakizungumza na EATV wamesema njia pekee ya kujikwamua kama taifa ni kuwa na maeneo ambayo yatazalishwa mazao ya kwa Kilimo Cha kudumu Ili kunusuru Hali ya ukame inapotokea.

Wamesema licha ya kupungua Kwa bei ya mafuta bado wanakutana na ushindani wa wafanyabiashara kutoka nje ambao huingia kununua nafaka Moja Kwa Moja kutoka kwa mkulima