Jumanne , 26th Apr , 2022

Wafanya biashara wa soko la msasani jijini Dar es Salaam wamesema mazingira ya soko lao Kwa sasa hayastahili kutokana na soko hilo kuwa na Miundombinu mibovu ya soko hilo pamoja na barabara zinazozunguka soko hilo.

Wakizungumza Kwa hisia kuhusu Hali ilivyo sokoni hapo wamesema ikinyesha mvua wateja wanashindwa kufika sokoni hapo kutokana na kuoza kwa barabara inayoingia sokoni hapo hali inayowafanya wateja kushindwa kufika kupata mahitaji.

"Ndugu mwandishi hii barabara yetu imekuwa kmaa zizi la ng'ombe wateja wanakuja wanashindwa kushuka kwenye magari njia haipitiki tope Kila mahali inawalazimu kuchukua wenyeji Ili kuwaagiza na hapa kufika sokoni hapa" Kulwa Abdalah Mfanyabiashara.

Wamesema kila mwaka viongozi wamekuwa wakifika na kuahidi kujengwa Kwa soko hilo lakini hawaoni utekelezaji licha ya wao Kuendelea kulipa ushuru na tozo mbalimbali.

"Kwa kweli mazingira ya hapa hayatuoendezi Mimi hapa Nina miaka mitatu sasa lakini hakuna kitu tuone kinafanyika mazingira yakiwa mazuri Kila kitu kitakaa sawa."alisema Baturi Abdalah,pamoja na Janeth Enock mfanyabiashara.

Kwa upande wake mzee Ali kambi Ali anasema Hali ya soko imekuwa mbaya kutokana na wateja kulalamika kushindwa kufika  hakuna maegesho ya magari.

"Hili soko linahudumia hadi watu wa masaki, Oysterbay na msasani yote lakini shida inakuja biashara zaidi hakuna ikinyesha mvua ndo kabisaaa hakuna biashara" Alisema Kambi Ali Kambi

Aidha William Mussa ambaye ni msafirishaji sokoni hapo anasema Kila anapofikisha wateja sokoni hapo wanashindwa kushuka kupata bidhaa kutokana na miundo mbinu mibovu  hasa kipindi Cha mvua.

"Mimi mwenyewe wateja ninao wafikisha hapa wanagoma kushuka inabidi akuandikie orodha ya vitu ukamchukulie sokoni,tuombe serikali kutazama soko hili ambalo limekuwa msaada mkubwa"alisema Williamu Musa Dereva Bajaji.