Ijumaa , 18th Nov , 2022

Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom imezindua kampeni yake inayofahamika kama #AmshaNdotoAmshaShangwe ambayo inalenga kutimiza ndoto za wateja wake kwa kushinda zawadi mbalimbali wakati akifanya miamala kwa kutumia M-pesa.

Mkurugenzi wa Biashara na Masoko wa Vodacom Linda Riwa

Mkurugenzi wa Biashara na Masoko wa Vodacom Linda Riwa, amesema kupitia kampeni hiyo ambayo imekuja msimu wa mwisho wa mwaka wateja wa Vodacom watashinda zawadi za fedha taslimu sambamba na wateja wa kila siku kujishindia milioni moja kila mmoja na smart TV