Jumanne , 9th Mei , 2023

Wizara ya Madini imeanza maandalizi ya Mpango Mkakati wa Miaka 10 wa Wizara hiyo ambapo Katibu Mkuu Wizara ya Madini Kheri Mahimbali, amekutana na kuzungumza na Washauri wa kodi jijini Dar es Salaam.

Katibu Mkuu Wizara ya Madini Kheri Mahimbali

Kikao hicho pia kimejadili kuhusu shughuli mbalimbali za uchimbaji wa madini zinazofanyika na matarajio ya Sekta ya Madini katika kipindi cha miaka 10 ijayo.

Mbali na Washauri wa kodi kampuni ya PricewaterhouceCoopers Limited (PWC), Deloitte Tanzania na KPMG, wengine waliohudhuria kikao hicho ni Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania  (GST) Dkt. Mussa Budeba.

Wengine ni Mkurugenzi wa Sera na Mipango Augustine Ollal, Kamishna wa Msaidizi wa Madini Maruvuko Msechu, Mkurugenzi wa Ukaguzi na Biashara ya Madini Tume ya Madini Venance Kasiki na Kaimu Meneja Uwekezaji na Mipango STAMICO Nsalu Nzowa.