
Bidhaa za vyakula zikiwa sokoni.
Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga, ameyasema hayo wakati akifunga maadhimisho ya siku ya chakula Duniani, ambayo kitaifa yamefanyika katika viwanja vya Mji Mwema, mkoani Njombe.
“Sekta ya kilimo imefanikiwa kuajili zaidi ya 65% ya nguvukazi na inachangia asilimia 30 ya pato la Taifa (GDP). Aidha, kilimo kinachangia takribani asilimia 65 ya malighafi za viwandani na asilimia 100 ya chakula kinachotumika nchini”, amesema Hasunga.
Hasunga, amesema kuwa Wizara ya Kilimo katika kipindi cha uongozi wa Rais Dkt. John Pombe Magufuli, imepata mafanikio makubwa ikiwamo kuchangia nchi kuingia mapema katika uchumi wa kipato cha kati mwaka 2019.