Jumanne , 25th Sep , 2018

Mtandao wa Facebook umetangaza listi ya makundi zaidi ya 115 dunia nzima yaliyoshinda katika programu yake maalumu inayojulikana kama ' Programu ya uongozi wa jamii, ndani yake ikiwa na raia sita kutoka nchini Kenya.

Makundi hayo sita yaliyo na raia wa Kenya yameifanya nchi hiyo kuwa ndiyo nchi pekee barani Afrika iliyoingiza makundi mengi zaidi katika listi hiyo.

Kila mmoja wa waliochaguliwa katika listi hiyo atazawadiwa kiasi cha dola 50,000 ambazo ni sawa na kiasi cha 114.3 millioni za kitanzania.

Katika kampeni ya kuwapata washindi hao kulikuwa na makundi ya aina mbili yaliyoshindanishwa, kundi la kwanza likiwa ni kundi la kiongozi bora wa kundi la kijamii katika eneo analoishi na kiongozi bora wa kundi la wafuasi kutoka sehemu mbalimbali.

Facebook pia imechagua watu watano kutoka kwenye makundi hayo 115 yaliyoshiriki ambao watajishindia kiasi cha dola 1,000,000 ambazo ni takribani 2.86 billioni za kitanzania kwaajili ya kuendeleza jamii zao.

Mmoja ya washindi wa programu hiyo raia wa Kenya ambaye ni mjasiliamali, Noar Nasiali aliyetengeneza kundi la wakulima zaidi ya 100,000 la bara la Afrika aliloliita "Klabu ya wakulima", ni raia pekee wa Afrika aliyeingia katika listi hiyo ya watu watano.

 Wakenya wengine waliokuwa katika listi ya makundi hayo 115 yaliyotangazwa ni Pamella Odour, Felister Wangari, Caroline Kihusa na Truphosa Mona ambaye ni mlemavu aliyeunda kundi la 'Women and Realities of Disabilitie (WARD)' katika mtandao huo akilenga kuongeza uelewa kwa wakenya kuhusu wanawake wanaoishi na ulemavu.