Jumatano , 27th Apr , 2022

Jamii imeaswa kufanya uwekezaji katika matumizi ya kidijitali hususani katika kizazi hiki ambacho kipo katika mabadiliko ya kasi ya teknolojia.

Rai hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa SAG group Edwin Bruno Mara baada ya kutembelea na kutoa msaada kwa kituo cha watoto yatima cha Mtambani kilichopo Kinondoni Dar es Salaam na baadae kushiriki katika Ifatar ya pamoja ikiwa ni sehemu ya ibada Kwa kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa Ramadhan.

"Sisi tunashirikiana na wadau wetu mbali kama Vodacom Tanzania katika upande wa mawasiliano kidijitali ili kuhakikisha kizazi Cha sasa kinapata Huduma hiyo na leo tumeamua kushiriki na watoto yatima wa mtambani kama ibada."alisema Edwin Bruno.

Awali Mkuu wa Kitengo cha masoko na Mauzo kutoka Vodacom Tanzania Warda Kimaro amesema Kwa muda sasa wamekuwa wakishirikiana na wadau wao SAG katika upande kuboresha mawasiliano ya kisasa Kwa jamii.

"Sisi kama Vodacom tunashukuru Kwa suala hili ambalo wenzetu wamelifanya Kwa watoto hawa ikiwa ni sehemu ya kurejesha furaha na kutambua uwezo na mchango watoto katika Dunia ya Sasa."alisema Warda.

Akimwakilisha na kutoa Salam za mufti mkuu wa Tanzania Sheikh Mkuu Wilaya ya ilala Adam Mwinyi Mkuu amesema kuwalisha yatima,kuwavisha ni thawabu huku akiwaka waislam kujiandaa na Sherehe za eid ambazo kitaifa zitafanyika Mkoani Dar es Salaam katika msikiti wa Bakwata Kinondoni.

"Mufti wetu anawaomba waislamu kote nchini kumaliza funga yao kwa amani utulivu akitoa shukrani kwa wote waliokumbuka kuwalisha wasiojiweza katika kipindi chote cha mwezi mtukufu. "alisema Sheikh Adam.pamoja shukrani kutoka Kwa mlezi wa kituo cha watoto yatima cha mtambani Immam Rajab Rajab.