Submitted by Anonymous on Jumatatu , 9th Jun , 2014
Jukwaa la Kili Music Tour likiwa tayari kwa shoo ndani ya viwanja vya CCM Kirumba Mwanza.
Mashabiki kutoka kila kona ya Mwanza wakiwa tayari kwa Tamasha la kili music tour 2014.
Mtangazaji wa Planet Bongo ndani EATV na EAR Dulla akiwa tayari kuendesha shoo nzima ya kili music tour Mwanza.
Mtangazaji wa Power Jams ndani EAR na FNL kwenye EATV Sam Misago akiwa tayari kuendesha show nzima ya Kili Music Tour Mwanza.
Mtangazaji wa Super Mix ndani EAR na Uswazi kwenye EATV Zembwela akiwa kwenye jukwaa na mashabiki wa kili music tour wakinena kuhusu tamasha hilo.
Msanii Ommy Dimpozi akiwa na wacheza shoo wake wakipozi kwa picha ya pamoja kabla ya kupanda kwenye jukwaa.
Msanii wa Ragga anayetikisa sasa Dabo Bado.
Dabo Bado juu ya jukwaa akionyesha njisi ya kucheza nyimbo za Ragga .
Msanii Vannesa Mdee akiwa na wacheza show wake wakitoa burudani ya nguvu kwa mashabiki wa mwanza.
Vannesa Mdee akionyesha manjonjo yake juu ya jukwaa.
Mashabiki wa Mwanza wakiburudika na tamasha la kili music tour 2014.
Msanii Mwasiti akitumbiza kwa mashabiki wake wa Mwanza.
Mwasiti akiimba kwa hisia nyimbo yake mpya "serebuka"
Rich Mavoko akipagawisha wakazi wa Mwanza katika tamasha la Kilimanjaro Music Tour.
Shangwe za wakazi wa Mwanza kwenye tamasha la kili music tour 2014
Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Ommy Dimpozi akipagawisha wakazi wa Mwanza katika show ya Kilimanjaro Music Tour iliyofanyika katika Uwanja wa Kirumba
Vanessa Mdee na Ommy Dimpoz wakimakinika katika show ya Kilimanjaro Music Tour iliyofanyika katika Uwanja wa Kirumba na kuwavutia maelfu ya mashabiki.
Ommy Dimpozi na Vanessa wakicheza nyimbo yao ya 'closer"
Msanii Christian Bella akitoa burudani ya nguvu ndani ya jiji la Mwanza kwenye tamasha la kili music tour 2014.
Msani wa muziki wa dance, Christian Bella akikonga nyoyo za wakazi wa Mwanza.
Msanii wa Bongo flava, Ben Pol akitumbuiza maelfu ya wakazi wa Mwanza wakati wa show ya Kilimanjaro Music Tour
Msanii wa miondoko ya Bongo flava, Young Killer akimtambulisha mama yake mzazi wakati wa show ya Kilimanjaro Music Tour iliyofanyika katika Uwanja wa Kirumba na kuwavutia maelfu ya mashabiki.
Wakazi wa Mwanza wakiwa wamefurika kwa maelfu huku wakishangilia ndani ya kiwanja cha CCM Kirumba.
Msanii wa Bongo Flava Izzo Biznez akifanya vitu vyake wakati wa show ya Kilimanjaro Music Tour.
Wasanii wa kundi kubwa la hip hop sana hapa Tanzania Weusi wakitoa burudani kwa mashabiki wao wa Mwanza.
Wakazi wa Mwanza wakiwa wamefurika kwa maelfu huku wakishangilia wakati kundi la Weusi likitumbuiza katika show ya Kilimanjaro Music Tour iliyofanyika katika Uwanja wa Kirumba na kuwavutia maelfu ya mashabiki.
Young Killer na Fid Q wakishirikiana kutoa burudani kwa wakazi wa Mwanza.
Wasanii kwa pamoja wakitoa shukhani kwa mashabiki wao wa Mwanza kwa kujitokeza kwa wingi kwenye tamasha la Kilimanjaro Music Tour iliyofanyika katika Uwanja wa Kirumba na kuwavutia maelfu ya mashabiki.