Amezaliwa siku ya mwaka mpya 1974 kijijini Misima Handeni Tanga
Mtoto wa saba kati ya watoto kumi na wawili.
Anatoka kwenye familia ya viongozi ambapo kaka yake aitwaye Zakari Hassan Doyo alikuwa mwenyekiti wa kijiji kwa miaka 15
Ana stashahada ya uandishi wa habari aliyoipata kwenye chuo cha Dar es Salaam City College
Alijiunga CUF akiwa na miaka 19 tu na mwaka 1996 akachaguliwa kuwa mwenyekiti wa CUF wilaya ya Handeni nafasi aliyohudumu kwa miaka 17
Alishiriki kuanzisha chama cha ADC na akamiliki kadi namba mbili ya chama hicho
2016 akawa Katibu Mkuu wa ADC hadi 2024
2024 alijiunga na NLD
Doyo Hassan Doyo ni Katibu Mkuu wa NLD
Muwekezaji kwenye sekta ya madini akiwa na migodi 54 iliyoajiri vijana 400
Anajishughulisha na kilimo cha zao la katani


















