Kesho Novemba 2 Yanga itakuwa uwanjani kukabiliana na Azam FC kwenye muendelezo wa michezo ya ligi kuu Tanzania bara kuna wasiwasi timu hiyo ikacheza mchezo huo bila Mabeki wa pembeni Yao Kuoassi na Shedrack Boka ambao ni majeruhi Nickson Kibabage naye akiwa hatihati kutokana na kupata maoumivu kwenye mchezo dhidi ya Singida Black Stars.
Naibu Waziri Mkuu, Dk. Doto Biteko (kushoto), akimsikiliza Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa GGML, Stephen Mhando (kulia) kuhusu teknolojia mpya zinazotumiwa katika uchimbaji wa kampuni hiyo mkoani Geita. Biteko alitembelea banda la GGML katika kongamano la Kimataifa la Madini na Uwekezaji Tanzania 2023 linalofanyika jijini Dar es Salaam