Wednesday , 15th Apr , 2015

Serikali imeombwa kuweka mkazo wa sheria katika suala la matumizi ya mitandao ya kijamii kwa wale wanaotumia kinyume na maadili.

Wanafunzi wa Mwaka wa Mwisho Chuo kikuu cha Ruaha Iringa wakipatiwa semina.

Wanafunzi wa chuo kikuu cha Ruaha mkoani Iringa wamesema kuwa watu wengi wameshindwa kutambua madhumuni ya matumizi ya mitandao ya kijamii na kupelekea kuweka picha za utupu katika mitandao hiyo.

Wanafunzi hao wamesema watu wanaotumia vibaya mitandao hiyo ni wale ambao wamesoma kutoka vyuo mbalimbali nchini.

Wamewataka watu wote wanaofanya vitendo hivyo kuwa na hofu ya Mungu kwani kufanya hivyo kunapelekea kuendelea kumomonyoa maadili kwa kizazi cha sasa na baadaye.

Hata hivyo, wamesema kama Serikali itatumia vizuri mswaada wa sheria iliyopitishwa hivi karibuni Bungeni mjini Dodoma kuhusu matumizi ya mitandao hiyo italeta ufanisi.