Tuesday , 21st Apr , 2015

Utendaji hafifu wa mashine za kujiandikishia vitambulisho vya uraia kwa wanafunzi wa vyuo vikuu mkoani irnga umechangia zoezi hilo kwenda taratibu.

Rais Jakaya Kikwete akionyeshwa mfano wa Kitambulisho cha Uraia.

Katibu wa serikali ya wanafunzi wa chuo kikuu cha Ruaha (RUCU)Ebenezer Rwabyo akizungumza kwa niaba ya wanafunzi amesema suala lingine ni kutokuwa na mawasiliano mazuri na wizara juu ya kuanza kwa zoezi hilo hali iliyochangia viambatanisho vingine kukosekana.

Kwa upande wake Mratibu wa zoezi hilo kutoka mamlaka ya usajiri wa vitambulisho vya taifa (NIDA) Daniel Katondo amesema zoezi hilo limeanza april 16 na limechukua siku saba na linatarajia kuhitimishwa kesho april 21.

Bw.Katondo amesema katika zoezi la uandikishwaji limekuwa na changamoto mbalimbali zikiwemo kukosekana kwa viambatanisho kwa Wanafunzi na watendaji wa mitaa kutoonyesha ushirikiano wa kupiga mihuri kwenye fomu.

Aidha ameongeza kwa kusema kuwa ambao hawata fanikiwa kujiandikisha wakati huu kutokana na kuwa zoezi hilo limepewa muda mfupi zoezi hilo bado ni endelevu hivyo watajiandikisha wakati mwingine.