Manispaa kuvifunga vituo vya Mwenge na Ubungo
Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam nchini Tanzania imetangaza rasmi kwamba inakusudia kukifunga kituo cha daladala cha Mwenge na kituo Kikuu cha mabasi cha Ubungo, na nafasi yake kuchukuliwa na kituo cha Makumbusho na kituo kipya cha Sinza.