Jaguar arudisha shukrani kwa Wafungwa
Staa wa muziki kutoka nchini Kenya, Jaguar kwa jina maarufu, kwa mara nyingine ameonesha moyo wake wa upendo kwa kuamua kurudisha shukurani katika gereza la Industrial Area huko Kenya, mahali ambapo alifanyia sehemu ya video ya ngoma yake ya 'kioo'.