Idadi kubwa ya wafanyakazi hulipwa ujira mdogo
Mwenyekiti wa shirikisho la vyama vya wafanyakazi Tanzania (Tucta) mkoa wa Mbeya, Alinanuswe Mwakapala, amesema idadi kubwa ya wafanyakazi wanalipwa mishahara chini ya kiwango na hawajajiunga na chama chochote cha wafanyakazi.