Misamaha ya kodi inazorotesha maendeleo - Mbunge
Fedha zinazopotea kutokana na misamaha ya kodi mbalimbali nchini Tanzania zimekuwa zikichangia kutofanikiwa kwa miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwa ni pamoja na ujenzi wa nyumba za walimu na madarasa ya shule za msingi na sekondari nchini.