Virusi vya Dengue vimeingia toka nje - IHI
Taasisi ya utafiti wa masuala ya afya na tiba ya Ifakara Health Institute imesema kuna uwezekano virusi vya homa hatari ya Dengue vimeingia nchini kutoka nchi za Asia na Amerika ya Kusini ambako ugonjwa huo upo kwa siku nyingi.