Nanyamba walia na tatizo la maji safi na salama
Wakazi wa halmashauri ya mji wa Nanyamba mkoani Mtwara wamelalamikia tatizo la uhaba wa maji lililodumu kwa miaka mingi kiasi cha kulazimika kusafiri umbali wa kilomita zaidi ya 50 mpaka Ruvuma kufuata huduma hiyo.

