Majeruhi wazidi kuiandama Liverpool

Mshambuliaji wa klabu ya soka ya Liverpool Jordon Ibe ataukosa mchezo wa leo wa kombe la FA dhidi ya Exeter City baada ya kupata majeruhi katika mechi iliyopita,

Ibe ambaye aliifungia bao la ushindi Liverpool dhidi ya Stoke city kwenye mechi ya mkondo wa kwanza wa kombe la ligi anaungana na wachezaji wengine saba wa kikosi cha kwanza cha klabu hiyo .

Kocha mkuu wa klabu hiyo Jurgen Klopp yupo kwenye wakati mgumu ikizingatiwa anamechi ngumu wikim ijayo ya ligi kuu ya soka nchini Uingereza dhidi ya vinara wa ligi hiyo klabu ya Arsenal.

Pages

Subscribe to East Africa Television RSS