Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Inspekta Jenerali(IGP), Ernest Mangu
Jeshi la Polisi nchini Tanzania limesema kuwa linaangalia uwezekano wa kukusanya na kuzichunguza silaha zote zinazomilikiwa na watu binafsi kwa lengo la kupambana na uhalifu hususani ujangili.