Miradi ya TEHAMA yatakiwa kushirikiana na Serikali
Taasisi za umma nchini zimetakiwa kushirikiana na Wakala wa Serikali Mtandao eGA katika kupanga na kutekeleza miradi ya TEHAMA serikalini ili kurahisisha mpango wa kubaini na kuondoa urudufu na kuipunguzia serikali gharama za uendeshaji mifumo.