Makamu wa Rais Suluhu kuhudhuria mkutano wa AU
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania SAMIA SULUHU HASSAN ataondoka nchini kesho jumamosi kwenda KIGALI nchini Rwanda kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano wa 27 wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa Umoja wa Afrika (AU).

