CAF yaitupa nje ES Setif ya Algeria
Klabu inayoiwakilishi wa Algeria katika kinyang'anyiro cha kuwania ubingwa wa vilabu barani Afrika, Klabu ya Entente Setif imetupwa nje ya mashindano hayo kutokana na mashabiki wa klabu hiyo kufanya vurugu wakati wa mechi dhidi ya Mamelodi Sundowns.