Jamal Malinzi, Rais wa TFF
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na shirikisho hilo, TFF inaunga mkono juhudi za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na juhudi za serikali kwa ujumla katika kuhakikisha vijana wa kitanzania wanakuwa na mazingira bora ya kupata elimu.
Kadhalika TFF inamshukuru Katibu wa Bunge, Dkt. Thomas Kashililah kwa juhudi za kuendeleza mpira wa miguu na kuutumia katika kuliletea taifa maendeleo.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania litaendelea kushirikiana na Ofisi ya Bunge Sports Club katika kufanikisha mashindano mbalimbali hasa mchezo wa hisani kati ya Simba Sports Club na Young African (Wabunge) utakaofanyika hapo baadaye kwa mujibu wa ratiba na uratibu wa Bunge.




