Sera Sekta ya Uvuvi itaikomboa Afrika-Hamad
Waziri wa Kilimo, Maliasili , Mifugo na Uvuvi wa Zanzibar, Mhe. Hamad Rashid Mohammed, amesema uwekwaji wa sera na mikakati ya pamoja katika sekta ya uvuvi kwa nchi za Afrika kutaweza kusaidia upatikanaji wa soko la uhakika la kimataifa.