Waziri awataka wananchi kulipia bili
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Gerson Lwenge amewashauri wananchi kuchangia gharama za maji ikiwa pamoja na ulipaji wa bili za maji kwa wakati ili waweze kupata huduma endelevu za maji safi na salama nchini.