FIFA kutoa mafunzo ya juu ya ukocha wa makipa TZ
Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu FIFA limeipa nafasi Tanzania kuwapa mafunzo ya juu ya ukocha wa makipa (Advanced Goalkeeping Coach Course) ikiandika historia kuwa nchi ya pili barani Afrika kwa makocha wa nafasi hiyo baada ya Botswana.
