Ahukumiwa miaka 30 jela kwa wizi wa pikipiki
Mahakama ya wilaya ya Mbarali Mkoani Mbeya imemhukumu kutumikia kifungo cha miaka 30 jela na kuchapwa viboko 12 mkazi wa Iyunga jijini Mbeya Salumu Ngasa maarufu kama Uncle Mkomavu (32) kwa unyang’anyi wa kutumia silaha.

