Rais Magufuli amlilia aliyekuwa RPC Singida
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemtumia salamu za rambirambi Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Ernest Mangu kufuatia kifo cha Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Singida SACP Peter Kakamba.