Watoto 60 waliopewa mafunzo ya kigaidi, wanaswa
Jumla ya watoto 60 wamekamatwa katika kipindi cha mwaka mmoja na Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam wakiwa wameachishwa masomo na kuingizwa katika mafunzo ya kigaidi ikiwemo kulenga shabaha kwa kutumia silaha na uporaji.