Serikali yaombwa kuboresha barabara Arumeru
Serikali imeombwa kuboresha miundombinu ya barabara na vituo vya afya wilayani Arumeru kwa lengo la kupunguza vifo vya mama na mtoto wakati wa kujifungua kwa kutembea umbali mrefu kwa ajili ya kupata huduma katika vituo vya afya maeneo ya vijijini.