Misri yashindwa kuifikia rekodi ya 1990
Timu ya kwanza kati ya tano za Afrika Misri, imekubali kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa Uruguay na kushindwa kulinda rekodi yake ya mwaka 1990 kwenye fainali zilizofanyika Italia ambapo kwenye mechi ya kwanza ilitoka sare ya 1-1 na Uholanzi.