
Misri imefungwa kwenye mechi iliyomalizika jioni hii ambapo imeruhusu bao la dakika za mwisho likifungwa na mlinzi wa kati wa Uruguay Jose Giménez kwa kichwa dakika ya 90.
Bao hilo limeiacha Misri kwenye wakati mgumu wa kufuzu hatua inayofuata ambapo italazimika kushinda mechi zake mbili zilizobaki katika kundi A dhidi ya Urusi na Saudi Arabia.
Katika mchezo mwingine wa kundi A hapo jana wenyeji Urusi ambao wapo kileleni mwa kundi hilo walitoa kichapo kikali cha mabao 5-0 kwa Saudi Arabia.
Misri leo imecheza bila ya nyota wake Mo Salah ambaye alikuwa benchi licha ya kuelezw akuwa amepona bega aliloumia kwenye mchezo wa fainali ya UEFA dhidi ya Real Madrid Mei 26.