Matokeo ya wanafunzi 333 yafutwa na 538 yazuiliwa
Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA), limefuta matokeo yote ya watahiniwa 333, waliofanya udanganyifu katika mitihani yao, ukiwemo mtihani wa upimaji wa Kitaifa wa Darasa la Nne(SFNA), mtihani wa kidato cha Pili (FTNA) na kidato cha Nne (CSEE).

