"Pancho amefariki wakati hatupo sawa"-Mabeste
Rapa Mabeste amesema alikuwa anatamani kuwepo na amani kati yake na marehemu Pancho Latino kabla ya kufariki, jambo ambalo linamuuma na linamfanya kuaamini hata yeye na waliobakia wanaweza kuondoka duniani muda wowote.

