Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa amejumuika na Waumini wengine wa Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu Bikira Maria Imaculata Chamwino katika Misa ya Jumapili ya Sikukuu ya Utatu Mtakatifu leo tarehe 7 Juni 2020.
Rais John Magufuli amewashukuru Viongozi wa Dini na Watanzania wote kwa kuitikia wito wa kumuomba mwenyezi Mungu aepushe janga la ugonjwa wa homa ya mapafu unaosababishwa na virusi vya Corona.