Madini ya Tanzanite makubwa yapatikana Mererani
Mchimbaji madini eneo la Mererani Laizer Kuryani, amepata mawe mawili ya Tanzanite yenye uzito mkubwa ,moja lina kilo 9.27 na jingine kilo 5.8 , ambapo serikali kupitia Benki Kuu, imeyanunua mawe hayo, kwa gharama ya Bilioni 7.8 . Kuryani ametambuliwa rasmi kama Bilionea.

