Katibu Mkuu amzungumzia Balozi Dkt Mahiga
Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Profesa Sifuni Mchome, amepongeza utendaji kazi wa aliyekuwa Waziri wa Katiba na Sheria Dkt Augustine Mahiga, na kusema kuwa alikuwa ni mnyenyekevu kwa kila mtu na alikuwa anatoa mawazo mbalimbali licha ya kwamba hakuwa ni Mwanasheria.