TFF yatoa maelezo matumizi ya Bil 2.3 za FIFA
Katibu Mkuu wa TFF Kidao Wilfred amesema Shirikisho la soka Duniani FIFA, kila mwaka wanaipa Tanzania Bil 2.3 ambazo hutoka kwa awamu mbili yaani Januari na Julai na huwa unafanyika ukaguzi wa matumizi ya awamu iliyopita kabla ya kupewa tena.