Joto lawatesa wachezaji wa Chelsea nchini Marekani
Kocha wa Chelsea Enzo Maresca amesema hali ya joto kali inayoendelea Philadelphia nchini Marekani imewapa wakati mgumu wa kufanya mazoezi yao ya mwisho kuelekea mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi dhidi ya Esperance utakaopigwa Juni 25 saa 10:00.