Rais Samia: 'Hata kama haumpendi Rais, vumilia tu'
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ametoa wito wa amani na uvumilivu kwa Watanzania wote, akiwataka Viongozi wa Dini na wananchi kwa ujumla kuepuka maneno na matendo yanayoweza kuvuruga utulivu wa nchi.

