Nigeria Yagomea mchezo kufuzu AFCON dhidi ya Libya

Timu ya Taifa ya Nigeria imepanga kugomea mchezo wa kufuzu AFCON 2025 Ugenini dhidi ya timu ya Libya. Kikosi cha Super Eagles kimeachwa uwanja wa Ndege kwa masaa 12 pasipo chakula wala maji ya kunywa, Wachezaji wamelazwa kwenye mabenchi ya Abiria huku mageti yakiwa yamefungwa na kutoa ugumu kwa timu ya Nigeria kuondoka uwanjani hapo.
Timu ya taifa ya Nigeria imepanga kugomea mchezo dhidi ya Libya kutokana na kufanyiwa vitendo ambavyo si vya kiungwana. Super Eagles ilitelekezwa uwanja wa Ndege kwa zaidi ya masaa 12 bila chakula wala maji na Wenyeji wao timu Taifa la Libya .