Timu ya Taifa ya Nigeria imepanga kugomea mchezo wa kufuzu AFCON 2025 Ugenini dhidi ya timu ya Libya. Kikosi cha Super Eagles kimeachwa uwanja wa Ndege kwa masaa 12 pasipo chakula wala maji ya kunywa, Wachezaji wamelazwa kwenye mabenchi ya Abiria huku mageti yakiwa yamefungwa na kutoa ugumu kwa timu ya Nigeria kuondoka uwanjani hapo.
Timu ya Taifa ya Nigeria ipo nchini Libya kucheza mchezo wa kufuzu AFCON 2025 itakayofanyika Morocco, kwa taarifa iliyotolewa na Nahodha wa kikosi cha Super Eagles zinasema Wametelekezwa uwanja wa Ndege kwa masaa zaidi ya 12. Mchezo wa Libya dhidi ya Nigeria unatarajiwa kuchezwa kesho siku ya Jumanne Oktoba 15, 2024.
Wanafainali wa AFCON iliyofanyika Ivory Coast Januari 2024, Wameachwa uwanja wa Ndege bila chakula na maji. Mageti ya uwanja wa Ndege yamefungwa hivyo kikosi cha Nigeria hakiwezi kutoka uwanjani hapo. Nigeria ilipaswa kutua uwanja wa Ndege wa Benghazi badala yake ndege yao ikatua uwanja wa Al Abraq umbali wa masaa matatu na nusu tokea sehemu ambayo walitakiwa kufikia.
Kumekuwa na matukio mengi ya nje ya uwanja katika mpira wetu wa Afrika na hili ambalo linaendelea nchini Libya kwa kikosi cha Nigeria ni maswala ambayo yanapaswa kukemewa kwa kiasi kikubwa. Troost- Ekong ambaye ni Nahodha wa Taifa lenye historia kubwa katika Mpira wa miguu Afrika amezungumzia uwezekano wa kugomea mchezo wao wa kesho.
Kitendo kisicho cha Ubiandamu kuwafungia Wachezaji uwanja wa Ndege bila chakula wala maji, Nahodha wa Libya Faisal Al-Badri naye amesema Wao pia walikutana na changamoto kama hiyo walipokwenda kuchezo wao wa kwanza dhidi ya Nigeria waliachwa uwanja wa Ndege bila taarifa yoyote kutoka kwa Wenyeji wao.
Shirikisho la Soka la Nigeria pamoja na Serikali ya nchi hiyo Wanaangalia uwezekano wa kuirudisha timu nchini kwao na kuugomea mchezo wa siku ya Jumanne usiku Oktoba 15. CAF wanapaswa kupitia ripoti ya tukio hili amesema William Troost- Ekong Nahodha wa Super Eagles Mchezaji wa zamani wa Watford ya Uingereza.
Mabingwa mara wa tatu wa AFCON wapo tayari kupoteza alama tatu ambazo watapewa Wenyeji waoWameweka wazi nia ya kutocheza mchezo huo dhidi ya timu ya Taifa ya Libya sababu ya vitendo visivyo vya Kibinadamu walivyofanyiwa nchini Libya.