Daniel Maldini awarithi Babu na Baba yake Italia

Daniel Maldini ameweka rekodi ya kuwa Mwanaukoo wa tatu kutoka Familia ya Wacheza Soka nchini Italia baada ya jana Oktoba 14, 2024 kwenye mchezo wa ligi ya Mataifa ya Ulaya dhidi ya timu ya Taifa ya Israel Daniel amefuata nyayo za Babu yake Cesare Maldini na Baba yake Paulo Maldini wote kuitumikia The Azzurri kwa vizazi vitatu tofauti.Cesare alianza kuitumikia Italia 1960,Paulo 1988 na Daniel 2024.
Mtoto wa Beki wa zamani wa timu ya Taifa ya Italia na klabu ya AC Milan Daniel Maldini amecheza kwa mara ya kwanza timu ya Italia. kwa kufanya hivyo ameendeleza tamaduni ya Ukoo wa Maldini kutumikia timu ya taifa Lao, Cesar Maldini alicheza miaka ya 1960, Paul Maldini 1985.