Monday , 1st Jun , 2015

Luteni Kalama, star wa muziki ambaye wiki iliyopita alimvisha pete ya uchumba rasmi mpenzi wake wa siku nyingi, mrembo aliyewahi kushikilia taji la Miss Ruvuma Bella amewahakikishia mashabiki wake kuwa hatua ya kufunga ndoa anayonuia kuichukua.

Luteni Kalama | Bella

Kukiwa na mifano dhahiri ya wasanii kadhaa walioshuka ama kuweka sanaa pembeni baada ya jukumu la ndoa na familia kuingilia kati, Luteni amesema kuwa kama kipaji cha mtu kipo hakiwezi kupotea, akijiamini kuwa jina la Luteni Kalama litabaki siku zote katika sanaa.

Wachumba hawa wapya bila kutaja tarehe rasmi wameiambia eNewz kuwa, Harusi yao itafanyika hivi karibuni.

Vile vile staa huyo akazungumzia ujio mpya wa kundi la Gangwe Mob, akiweka wazi kuwepo kwa rekodi kama 3 ambazo zitatoka kati ya sasa na mwezi wa 7.