Friday , 1st May , 2015

Michuano ya kombe la muungano kwa mchezo wa mpira wa miguu inatarajiwa kuanza kutimua vumbi Mei 10 mwaka huu uwanja wa Igowole, Mufindi mkoani Iringa.

Akizungumza na East Africa Radio, Mratibu wa michuano hiyo, Daud Yassin amesema, mashindano hayo yatashirikisha timu 10 zikiwamo tisa kutoka Tanzania Bara na moja kutoka Zanzibar lakini mpaka sasa hawajajua ni timu gani.

Yassin amesema, timu shiriki katika michuano hiyo kutoka mkoani Iringa ni Mucoba, Mtwivila, Incoment, Changarawe na Igowole.

Yassin amesema timu nyingine ni Azam B ya jijini Dar es salaam, Mbaspo na Mbeya City B za jijini Mbeya pamoja na Dodoma FC.